المدة الزمنية 24:36

MUSTAKBALI WA WAYAHUDI KWA MUJIBU WA QUR'AN TUKUFU - SHEIKH SULEIMAN KILEMILE - PART 1

بواسطة Rashid Dilunga
12 184 مشاهدة
0
77
تم نشره في 2015/01/07

Kwa karne nyingi watu hawa hawakuwa wakijulikana kama Wayahudi, bali walijulikana kama wana wa Israel (au wana wa Nabii Yakub) kama wanavyotajwa ndani ya Qur'an. Ni wale tu ambao walijitangazia utaratibu wa maisha unaofuata matakwa ya walimu wao wa Sheria, Mfumo ambao ndio wa Kiyahudi na wafuasi wake wakaitwa Wayahudi (yaani wafuasi wa dini ya Kiyahudi) Kabla ya ujio wa Nabii Isa (AS), Wayahudi waligawanyika makundi mawili. Kuna walioamua kuufuata utaratibu wa kuiheshimu Siku ya Sabato, amri iliyoachwa na Nabii Musa ndani ya Torati. Kundi hili ambalo ndilo kubwa likaitwa la Wasabian (Sabiin) ndani ya Qur'an. Na baada ya ujio Nabii Isa na kuondoka kwake, lilipatikana kundi jingine lililoitwa la Manasara (Wakristo) Lakini kuanzia karne ya 13, kwa ujumla walianza kuitwa Wayahudi kutokana na neno la Kirumi la Judea, lililomaanisha eneo walilopewa kukaa kabila moja la Yuda iliko Yerusalemu. Kabila hili miongoni mwa makabila 12, ndilo lililokuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru wa kujitawala kutoka kwa watawala wao Warumi. Hadi Mtume Muhammad (S.A.W) anahamia mjini Madina, tayari aliyakuta baadhi ya makabila ya Kiyahudi, yaliyokuwa yamelowea katika eneo hilo. Kuhamia kwa Wayahudi mjini Madina na sehemu nyingine za Waarabu kulitokana na sababu kadhaa na miongoni mwazo mbili ndizo huwa zinapewa umuhimu. Sababu ya kwanza, inasemekana kwamba Wayahudi walikuwa wanatarajia ujio wa Nabii mwingine atakayekuwa na nguvu ya kuwakomboa Wayahudi kutokana na kutawaliwa na Dola za kigeni, na kwamba kulikuwa na dalili katika maandiko yao, za Nabii yule kutokea katika nchi za Mashariki. Hivyo baadhi ya makabila ya Kiyahudi yalihamia mashariki katika ardhi za Waarabu wakidhani kuwa kama Nabii huyo atakapotokea basi atokee katika mojawapo ya kabila zile za kihamiaji. Sababu ya pili ni kwamba katika mwaka 70 AD, Jenerali wa Kirumi aliyeitwa Titus, alipigana na Wayahudi na kufanikiwa kuiteka Yerusalemu na hivyo kukomesha utawala wa Kiyahudi katika ardhi ya Wapalestina. Kufuatia hali hii wengi katika makabila ya Kiyahudi hawakupenda kutawaliwa wakihofia maisha yao, walikimbia na kuhamia katika nchi za Kiarabu na kuyakalia mabonde yenye rutuba kwa ajili ya kilimo na biashara. Kwa hatua hii wakawa walowezi katika nchi za Waarabu. Hadi mwanzoni mwa karne ya 7, makabila matatu ya Kiyahudi yalishaweka makazi yao mjini Madina, wakati ule ikiitwa Yathrib. Mji huu uliitwa Madina (Madinatun-Nabiy) baada ya ujio wa Mtume Muhammad (S.A.W) kwa heshima yake. Msuguano kati ya Waislam na Wayahudi, ulianza baada ya Mtume kuhamia Madina. Kadiri alivyoendelea kuwa maarufu na kukubalika kama Kiongozi wa umma, ndivyo ilivyozidi chuki ya baadhi ya Wayahudi dhidi yake. Kuna waliomkubali, na kuna wengine waliomkataa waziwazi na wengine kwa kujificha (wanafiki). Kwa kuwa Mtume alilenga katika kuijenga jamii yenye kufuata misingi ya amani, haki na usawa, Wayahudi walimuona kuwa ni tishio dhidi ya maslahi yao yaliyotokana na mufumo wao wa kinyonyaji. Pia kwa kuwa alikuwa ni Mtume, walikuwa wakimpinga na kuhojiana naye kutokana na kuzikosoa baadhi ya tafsiri za maandiko yao, wakisema hakuwa na maarifa juu ya mambo ya kiroho. Lakini kutokana na kushindwa kwao kuitoa kosa Qur'an, wengi wa Wayahudi wa Madina walimuona Muhammad kama Mtume wa kweli na kuamua kusilimu na kumfuata, licha ya wengine kuendeleza ubishi wao na mashaka. ......Sasa fuatana na Sheikh Suleiman Kilemile kutoka Tanzania, katika Mada hii inayowahusu Wayahudi...

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 15