المدة الزمنية 5:3

AHADI SITA ZA BWANA YESU KUHUSU MAOMBI

بواسطة SIRI ZA BIBLIA
4 231 مشاهدة
0
65
تم نشره في 2021/03/30

#YesuKristo#Maombi#Imani#Wokovu 1. Mathayo 18:19,20 “Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao” Nampenda Bwana Yesu. Yani kila tukutanikapo wanadamu wawili huwa si wawili tena bali tupo watatu. Maana Bwana Yesu hujihudhurisha kuja kuchukua maombi yetu ampe Baba. 2. Marko 11:22-24 “Yesu akajibu, akamwambia, Mwaminini Mungu. Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake. Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu” 3. Yoh. 14:13,14 ‘Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya’ Msisitizo: – Bwana Yesu anasema lolote tutakaloomba! 4. Yoh. 15:7 “Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. ” Kukaa ndani ya Kristo na maneno yake kukaa ndani yetu huo ni ushirika katika mahusiano yetu na Mungu. Ni ushirika wa kudumu. Ushirika wa kila siku. Ni ushirika ambao ulianzishwa pale msalabani na Kristo mwenyewe. Damu yake ilipomwagika pale msalabani kwa ajili ya kutusafisha dhambi zetu, ilianzisha mahusiano yasiyo na kikomo. Kumuamini Bwana Yesu na kumkiri kama Bwana na Mwokozi wa maisha yetu ni mwanzo wa mahusiano hayo ya kudumu katika Kristo. Kuokoka ni hatua ya mwanzo. Na tunapaswa kuendelea na mahusiano na Kristo kwa Roho Mtakatifu. 5. Yoh. 15:16 “Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni” 6. Yoh 16:23,24 “Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu. - Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu. -” Hakuna masharti ya NINI TUOMBE ila kuna masharti ya NAMNA YA KUOMBA: i. Kupitia jina la Yesu ii. Mtu aombaye awe na mahusiano na Mungu iii. Mwombaji awe na Imani Ubarikiwe sana.

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 13