المدة الزمنية 1:58

Genge la wahalifu lakamatwa baada ya kuvamia wananchi eneo la Gichugu, Kirinyaga

بواسطة Citizen TV Kenya
13 486 مشاهدة
0
82
تم نشره في 2021/06/30

Maafisa wa polisi kutoka eneo la Gichugu Kaunti ya Kirinyaga wamewatia nguvuni vijana kumi na mmoja wanaojihusisha na genge la uhalifu linalojulikana Kama "Wisame " Kulingana na kamanda wa polisi eneo hili Anthony Mbogo genge hili lilikuwa na lengo la kuwasajili wanafunzi kutoka chuo kikuu cha Kirinyaga katika vitendo vya uhalifu. Wazazi sasa wakitakiwa wafuatilie mienendo ya watoto wao ili kuwazuia kujiunga na makundi ya kigaidi kupitia ueneaji bewa itikadi kali. Kamishena wa Kaunti ya Kirinyaga Jimmy Njoka amesema kuwa vijana wengi wamejihusisha katika uraibu wa mihadarati. Polisi wamegundua kuwa watoto wadogo kuanzia umri wa miaka kumi na sita wameanza kutumia dawa za kulevya na kisha kujiunga na kundi hili huku Mbogo akisema wamefanikiwa kukabiliana na uraibu huu.

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 14