المدة الزمنية 48:49

Zitto Kabwe: Hili la Wamachinga Linanisononesha Sana

بواسطة The Chanzo
1 377 مشاهدة
0
16
تم نشره في 2021/12/02

Hii ni sehemu ya pili ya mahojiano maalum kati ya The Chanzo na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe yaliyofanyika nyumbani kwake jijini Dar es Salaam mnamo Novemba 27, 2021. Kwenye sehemu hii, Zitto Kabwe, ambaye alipata kuwa mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini kwenye Bunge la 11, anafafanua mgogoro unaoendelea hivi sasa nchini Ethiopia baina ya jeshi la nchi hiyo na wanamgambo wa TPLF ambao mpaka sasa umegharimu maelfu ya maisha ya raia wa Ethiopia na kuwafanya wengine wengi kukimbilia uhamishoni. Zitto anatueleza kiini cha mgogoro huo na kipi anadhani kinapaswa kufanywa kurejesha hali ya utulivu nchini humo, akisisitiza umuhimu wa majadiliano katika juhudi za utafutaji wa suluhu. Pia, anaeleza tathmini yake ya juhudi zinazofanywa na Umoja wa Afrika katika kuleta amani nchini humo pamoja na nini Tanzania kama nchi inaweza ikafanya kuchochea juhudi hizo. Kwenye sehemu hii pia ya mahojiano yetu na Zitto, mwanasiasa huyo anaeleza tathmini yake ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na takribani miezi 10 tangu achukue hatamu za kuliongoza taifa la Tanzania hapo Machi 19, 2021. Zitto anaeleza unafuu wa kisiasa uliokuja na uongozi wa Rais Samia, akisema angalau sasa hatembei akiangalia nyuma kama kuna mtu anamfuata. Hata hivyo, mwanasiasa huyo anaeleza kusikitishwa na baadhi ya hatua ambao Serikali ya Rais Samia imezichukua ambazo anadhani zinawarejesha nyuma Watanzania kisiasa na kiuchumi. Hatua hizi ni pamoja na uamuzi wa Serikali kumfungulia mashtaka ya ugaidi Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe; Samia kusita kukutana na viongozi wa vyama vya siasa licha ya kuahidi kufanya hivyo; pamoja na uhamishaji wa wamachinga kutoka kwenye maeneo mbalimbali ya miji kwa kile mamlaka inakiita ni ‘kuwapanga.’ #TheChanzo

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 3