المدة الزمنية 7:43

CCM SHINYANGA YAKAMILISHA MCHAKATO WA KURA ZA MAONI, MAIGE, LEMBELI NA DC MSTAAFU KATAMBI

بواسطة KAHAMA TV ONLINE
1 859 مشاهدة
0
8
تم نشره في 2020/07/23

MCHAKATO wa upigaji kura za maoni kwa watia nia wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Shinyanga wanao omba kuchaguliwa kugombea nafasi ya ubunge katika majimbo ya sita yaliyopo katika mkoa huo umekamilika rasmi. Matokeo ya kura hizo yametangazwa rasmi huku mmoja wa wabunge wanaotetea nafasi zao katika Jimbo la Msalala wilayani Kahama, Ezekiel Maige akiangushwa baada ya kupata kura 118, mshindi katika kura hizo ni Idd Kassim aliyepata kura 327 ambapo kwa Jimbo la Kahama, Jumanne Kishimba ameshinda kwa kupata kura 234 huku aliyewahi kuwa mbunge wa Jimbo hilo James Lembeli akiambulia kura 54. Msikilize hapa Katibu wa CCM wa mkoa wa Shinyanga, Donald Magessa akitoa taarifa ya matokeo ya uchaguzi wa kura za maoni zilizopigwa kwenye majimbo mengine ya mkoa wa Shinyanga.

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 0