المدة الزمنية 4:14:3

KKKT USHARIKA WA KIJITONYAMA: IBADA YA KUHITIMISHA MAFUNGO YA SIKU 40 DEC 18, 2020

16 196 مشاهدة
0
279
تم نشره في 2020/12/18

KKKT USHARIKA WA KIJITONYAMA IBADA YA KUHITIMISHA MAFUNGO YA SIKU 40 DEC 18, 2020 SOMO: KUHITIMU NYAKATI NGUMU UKOMO WA UKIWA WA YERUSALEMU MEPHIBOSHETH ECONOMIC & FINANCIAL FREEDOM 2 Wakorintho 2 : 14 Nehemia 8 : 10 2 Samweli 9 : 1 - 13 Mwanzo 15 : 13 - 14 Hosea 6 : 1 - 3 2 Wakorintho 2 : 14 14 Ila Mungu ashukuriwe, anayetushangiliza daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu. Nehemia 8 : 10 10 Kisha akawaambia, Enendeni zenu, mle kilichonona, na kunywa kilicho kitamu, tena mpelekeeni sehemu yeye asiyewekewa kitu; maana siku hii ni takatifu kwa Bwana wetu; wala msihuzunike; kwa kuwa furaha ya Bwana ni nguvu zenu. 2 Samweli 9 : 1 - 13 1 Kisha Daudi akasema, Je! Amesalia mtu mmoja katika nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema kwa ajili ya Yonathani? 2 Palikuwa na mtumishi mmoja wa nyumba ya Sauli, jina lake Siba, basi wakamwita aende kwa Daudi; na mfalme akamwuliza, Wewe ndiwe Siba? Naye akasema Mimi, mtumwa wako ndiye. 3 Mfalme akasema, Je! Hakuna hata sasa mtu ye yote wa nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema ya Mungu? Siba akamwambia mfalme, Yonathani anaye mwana hata sasa, aliye na kilema cha mguu. 4 Mfalme akamwambia, Yuko wapi? Siba akamwambia mfalme, Tazama, yumo katika nyumba ya Makiri, mwana wa Amieli, katika Lo-debari. 5 Basi mfalme Daudi akatuma watu, akamwondoa katika nyumba ya Makiri, mwana wa Amieli, katika Lo-debari. 6 Basi Mefiboshethi, mwana wa Yonathani, mwana wa Sauli akaenda kwa Daudi, akaanguka kifudifudi, akasujudu. Daudi akasema, Mefiboshethi! Naye akaitika, Mimi hapa, mtumwa wako! 7 Daudi akamwambia, Usiogope, maana bila shaka nitakutendea mema; kwa ajili ya Yonathani, baba yako, nami nitakurudishia mashamba yote ya Sauli, baba yako; nawe utakula chakula mezani pangu daima. 8 Akasujudu, akasema, Mimi mtumwa wako ni nini, hata ukamwangalia mbwa mfu kama mimi? 9 Ndipo mfalme akamwita Siba, mtumwa wa Sauli, akamwambia, Mali yote yaliyokuwa ya Sauli na ya nyumba yake nimempa mwana wa bwana wako. 10 Nawe utamlimia nchi hiyo, wewe, na wanao, na watumwa wako; nawe utamletea mwana wa bwana wako matunda yake, apate chakula ale; lakini Mefiboshethi, mwana wa bwana wako, atakula chakula mezani pangu sikuzote. Basi huyo Siba alikuwa na wana kumi na watano na watumwa ishirini. 11 Ndipo Siba akamwambia mfalme, Mimi, mtumwa wako, nitatenda hayo yote kama bwana wangu, mfalme, alivyoniamuru. Na kwa habari za Mefiboshethi, mfalme alisema, Atakula mezani pangu, kama mmojawapo wa wana wa mfalme. 12 Huyo Mefiboshethi alikuwa na mwana mdogo, jina lake akiitwa Mika. Na watu wote waliokaa nyumbani mwa Siba walikuwa watumwa wa Mefiboshethi. 13 Basi Mefiboshethi akakaa Yerusalemu; maana alikuwa akila chakula sikuzote mezani pa mfalme; naye alikuwa na kilema cha miguu yote miwili. Mwanzo 15 : 13 - 14 13 Bwana akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa muda wa miaka mia nne. 14 Hata na taifa lile, watakaowatumikia, nitawahukumu; baadaye watatoka na mali mengi. Hosea 6 : 1 - 3 1 Njoni, tumrudie Bwana; maana yeye amerarua, na yeye atatuponya; yeye amepiga, na yeye atatufunga jeraha zetu. 2 Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, nasi tutaishi mbele zake. 3 Nasi na tujue, naam, tukaendelee kumjua Bwana; kutokea kwake ni yakini kama asubuhi; naye atatujilia kama mvua, kama mvua ya vuli iinyweshayo nchi. Mhubiri: Mch. Dkt. Eliona Kimaro Kwa maombi na ushauri: Mch. Dkt. Eliona Kimaro. Simu :+255655516053, +255754516053 YouTube : Rev. Dr. Eliona Kimaro TV Barua Pepe: elionakimaro555@gmail.com

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 26