المدة الزمنية 21:1

LIVE: GLOBAL HABARI JUNI 25 - RAIS ATANGAZA CORONA TANZANIA

بواسطة Global TV Online
2 635 مشاهدة
0
16
تم نشره في 2021/06/25

🔴#LIVE: GLOBAL HABARI JUNI 25 - RAIS ATANGAZA CORONA TANZANIA... Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema tayari kuna wagonjwa wa Covid-19 ambao wamebainika nchini katika wimbi la tatu la ugonjwa huo na kuwataka viongozi wa dini kuwaelekeza waumini kuchukua tahadhari. Rais Samia ameyasema hayo leo wakati akizungumza na Maaskofu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kwenye makao yao makuu yaliyopo Kurasini, jijini Dar es Salaam. Rais Samia ameeleza kuwa kinga ni bora kuliko tiba na ni muhimu kwa watu kuendelea kutumia kila kinachoelekezwa kuwa kinga ya maradhi hayo ili kuliepusha taifa na vifo. Hii ni mara ya kwanza kwa Serikali ya Tanzania kutoa taarifa za kuwepo kwa maambukizi ya corona nchini kwani mara ya mwisho kutoa takwimu za ugonjwa huo ilikuwa Mei, 2020. Aidha Rais Samia ametumia fursa hiyo kulipongeza Kanisa Katoliki pamoja na dini zote kwa mchango wake mkubwa katika kujenga taifa. Naye Askofu Mkuu na Rais wa TEC, Gervas Nyaisonga ameeleza kuwa kanisa katoliki linamuunga mkono Rais Samia na katika sera ya elimu kanisa hilo limekuwa mstari wa mbele katika uanzishaji wa shule mbalimbali kwa lengo la kutoa huduma hiyo na si kufanya biashara. ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx ⚫️ VISIT AMAZON: https://www.amazon.com/shop/globaltvonline ⚫️ JE, NA WEWE UNA HABARI? ⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE ( +255 784 888982), ( +255 713 837506) ⚫️ Email: globaltvbest@gmail.com OR abbymrisho@gmail.com ⚫️ OUR PLAYLISTS: ⚫️ HABARI MPYA DAILY:shorturl.at/mnux2 ⚫️ HISTORIA ZA VIONGOZI ZA KUSISIMUA: http://bit.ly/mikasa_ya_kusisimua ⚫️ GLOBAL RADIO TV: http://bit.ly/255globalradio ⚫️ EXCLUSIVE INTERVIEW: http://bit.ly/exclusive_interviews ⚫️ Subscribe Global TV http://bit.ly/globaltvonline

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 4