المدة الزمنية 21:37

SIMBA SC 2-1 KMC FC; HIGHLIGHTS (TPL - )

بواسطة Azam TV
197 340 مشاهدة
0
511
تم نشره في 2018/12/19

Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba SC wamepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya KMC katika mchezo wa ligi hiyo uliopigwa jioni ya leo kwenye Dimba la Taifa Dar es Salaam. Simba walipata mabao yao mawili ndani ya dakika 14 za kwanza, wakitumia dakika mbili pekee, la kwanza likifungwa na Adam Salamba dakika ya 12 na la pili likifungwa na Said Ndemla dakika ya 14. Simba ilitawala zaidi kipindi cha kwanza, huku KMC wakiingia kwa nguvu zaidi kipindi cha pili kwa mashambulizi mfululizo na kufanikiwa kupata bao la kufutia machozi dakika ya 68 kupitia kwa James Msuva. Beki mpya wa Simba, Zana Coulibary ameichezea timu yake kwa mara ya kwanza baada ya kusajiliwa katika usajili wa dirisha dogo kama ilivyokuwa kwa Elias Maguli wa KMC. Matokeo hayo yameifanya Simba kufikisha pointi 30 ikiendelea kusalia katika nafasi yake ya tatu, nyuma ya Azam FC wenye pointi 40 na Yanga wenye pointi 44. Ligi itaendelea kesho Alhamisi kwa mchezo mwingine wa kiporo kati ya African Lyon dhidi ya Yanga utakaopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 125