المدة الزمنية 9:15

KWA NINI MATITI HUUMA/KUWASHA KWA MJAMZITO | SABABU ZA MATITI KUUMA KWA MJAMZITO

بواسطة Dr. Mwanyika
24 709 مشاهدة
0
188
تم نشره في 2022/01/08

MAUMIVU YA MATITI KATIKA KIPINDI CHA UJAUZITO. Baadhi ya Wanawake hupata Maumivu ya Matiti ktk kipindi cha Ujauzito. Dalili hii huaanza kutokea Mimba inapofikisha Wiki 2 za Ujauzito kipindi ambacho Baadhi ya akina Mama Wajawazito huwa hawajajigundua kuwa wao ni Wajawazito na pia huendelea kuwepo kwa Miezi Mitatu ya Mwanzoni mwa Ujauzito huweza kupungua Miezi Mitatu ya katikati mwa Ujauzito na Kujitokeza Tena Miezi Mitatu ya Mwishoni mwa Ujauzito. Tafiti zinaonesha Wajawazito 17 Kati ya Wajawazito 100 huwa na Dalili hii ya Maumivu ya Matiti ktk kipindi cha Ujauzito. Maumivu ya Matiti ktk kipindi cha Ujauzito hutofautiana kati ya Mjamzito Moja na Mwingine kuna baadhi huwa na Maumivu kidogo na wengine huwa na Maumivu Makali zaidi mpaka kushindwa kufanya kazi zao za kawaida bila Matibabu. Hali hii huweza kujitokeza kwenye Titi au Ziwa Moja au Matiti yote Mawili. DALILI ZA MAUMIVU YA MATITI KATIKA KIPINDI CHA UJAUZITO. Mjamzito mwenye Hali hii huwa na Dalili zifuatazo; 1. Maumivu ya Matiti au Titi moja ambayo huwa kama Sindano zinachoma choma. 2. Maumivu Makali wakati wa Kujishika Matiti au Titi liloathirika. 3. Matiti kuongezeka Msisimko ambao si wa kawaida. 4. Maumivu kama Maumivu ya Kidonda kwenye Ziwa au Matiti yote Mawili. 5. Maumivu huweza kuuma kwenye Chuchu au Kuuma kuelekea kwenye Kwapa katika upande ambao Ziwa au Matiti yanauma. VISABABISHI VYA MATITI KUUMA KTK UJAUZITO. 1. Ongezeko la Homoni ya Estrogeni na Progesterone hususani kwenye Miezi Mitatu ya Mwanzoni mwa Ujauzito. Katika kipindi cha Mwanzoni mwa Ujauzito Kutokana na Ongezeko la Homoni ya Estrogeni hupelekea kuongezeka kwa Mishipa ya Damu na Vimirija vya Maziwa hali hii hupelekea Maumivu kwa Mjamzito. Kuna Baadhi ya Wanamke huweza kupata hali hii Siku chache kuelekea Hedhi yao ya kawaida ni Kutokana na Ongezeko la hizi Homoni za Progesterone na Estrogeni. 2. Ongezeko la Homoni ya Prolactin na Oxytocin ambazo hutolewa na Tezi ya Pituitari kwenye Miezi Mitatu ya katikati na Mwishoni mwa Ujauzito ambazo huuanda Mwili na Matiti kwa ajili ya utengenezwaji wa Maziwa ya Mtoto hupelekea Baadhi ya mabadiliko na Kuongeza kwa Mirija ya Maziwa kwenye Matiti na kupelekea Maumivu ya Matiti ktk kipindi cha Mwishoni mwa Ujauzito. 3. Uvaaji wa Brazia zisizobana na kushikiza Matiti vizuri. Matumizi ya Brazia ambazo si za Wajawazito kwenye kipindi cha Ujauzito huweza kupelekea Ongezeko kubwa la Maumivu ya Matiti kwa sababu hushikiza vibaya Matiti na kuachia sehemu nyingine za Matiti zikining'inia Vibaya na kupelekea Maumivu ya Matiti ktk kipindi cha Ujauzito. Hususani kwa Wajawazito wenye Matiti Makubwa Sana. MAMBO YAKUFANYA ILI KUPUNGUZA MAUMIVU YA MATITI KATIKA KIPINDI CHA UJAUZITO. 1. Vaa Brazia Nzuri zilizotengenezwa na Pamba ambazo zina Mikanda Mipana ya mabega na zinazoshikiza Maziwa au Matiti vizuri bila kuachia Baadhi ya sehemu za Matiti kwa Nje na kufanya Matiti kuning'inia, hii huweza kusaidia kupunguza Maumivu ya Matiti ktk kipindi cha Ujauzito, NB; Hususani kwa Wajawazito wenye Matiti Makubwa Sana. 2. Acha Tabia ya Kujishika Maziwa/Matiti au Kukamua Maziwa/Matiti yako kipindi ambacho yanakuwa yanauma, Kitendo Cha Kujishika shika Matiti hupelekea inflamesheni na Maumivu kuongezeka katika kipindi chako Cha Ujauzito. NB: Hii unapaswa kumwambia na mwenza wako ili aelewe Kitendo Cha Kushika Matiti huongeza hali ya Maumivu katika Kipindi cha Ujauzito kwa Mjamzito mwenye Maumivu ya Matiti ktk Ujauzito wake. 3. Unaweza kukanda Matiti yako kwa Maji ya Barafu na Kitambaa laini au Barafu ili kupunguza Maumivu ya Matiti ktk kipindi chako Cha Ujauzito na Endapo Maumivu yanazidi unatakiwa kuwahi hospitali kwa ajili ya Kuonana na Daktari na kuandikiwa Dawa za Maumivu. 4. Unatakiwa kuonana na Daktari endapo unapata Maumivu ya Matiti na pia unaona au kuhisi Dalili zifuatazo; Matiti kutoa Uchafu wenye harufu Mbaya au Damu, Uvimbe kwenye Matiti yako, Kujikunja kwa Ngozi ya Titi kwa Kuingia au Chuchu kuingia Ndani kusiko kawaida, Kubadilika rangi ya Ziwa kuwa Nyekundu au Njano kama Chungwa. Nifuatilie kwenye channel yangu kuhusu Mambo ya Ujauzito. /c/DrMwanyika Nifuatilie Instagram kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://www.instagram.com/dr._mwanyika/ Nifuatilie kwenye website hii kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://mamaafya.com/ Nifuatilie kwenye Facebook page kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://www.facebook.com/JapideAfya/ Usisahau kudownload app ya Mama Afya Bora kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://play.google.com/store/apps/details?id=com.wapnum.mamaafyaapp #MatitiKuuma #DrMwanyika #MamaAfya

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 131
  • @
    @miriamkarata74952 years ago Mungu akubariki daima doctor, Asantee sana 4
  • @
    @jacklinekayombo4682 years ago Asante doctor japo nmechelewa kukujua na kukufwatilia 2
  • @
    @jenifferassenga3617 months ago Hallo naomba kuuliza Dr,
    Mimi n mjamzito week 21 sasa, ziwa langu la kulia linatoa maji na haliumi, yaan maumiv nnayoskia n ya kawaida tu kwenye chuchu lbda nikijiparuza na nguo au mkono. Lakn tofaut na hapo sna maumivu makubwa ya kutisha.. ila ziwa lnatoa maji yanatiririka kabisa.. usiku wa kuamkia leo hadi shuka limeloa kabsa kbsaa maji, Je naweza kua na tatzo ama n mabadiliko ya kawaida? ...
    1
  • @
    @srpriscasilayo86842 years ago Namhudumia mgonjwa amekuja na ujauzito 20wks maziwa yamejaa na yanauma sana. Prime gravida! 1
  • @
    @elizalyanda98282 years ago Minakushukuru Sana Yani umekuwa ukinisaisia Sana lakini yanaweza kutuli mda frani maana minaona nilipo funga miezi 3 yamepunguwa kuuma 1
  • @
    @motiontz3722last year Doctor naomba msaada kdgo!! Tangu mwez wa pili mke Wang tar19 alienda blid lkn ilikuwa tofaut kdg maana yalitoka matone ya dam kdg xana afu yamemix na utelez kdg,,, ilitokea ni siku mbili tu tang hapo hajaona siku zake mpka sasa.... Lkn anajiskia mdomon mchungu pia chuchu zinamuuma saana hata chakula hajiskii kula je inaweza ikawa ni mimba???🙏🙏 ... 1
  • @
    @user-pd8nq6ks6e3 months ago asante doctor ila mim pemben ya chuchu kumekuw kwekundu sasa sijajua sababu ya kujikuna ? au 1
  • @
    @shufaamakame58392 years ago Mm doctor matti yangu yamevimba sn afu chuchu ndio zinatonesha htr hdi nawaza nikijifunguwa nitanyonyeshaje mn km yana vidonda na ht hayana kidonda.naomba ushauri wko 2
  • @
    @evelinemshana7466last year Mm Dr nina ujauzito wa week 26 ziwa la upande wa kulia linauma sana kwa ndani nasikia kuchomwa chomwa na kuna vimbegu NIKIGUSA VINAUMA ILA CHUCHU NIKIVUTA INAKUJA JUU KAWAIDA JE KUNA SHIDA? 1
  • @
    @lunahsalum38922 years ago Mimi nina maumivu ya maziwa wiki ya pili hiii numepima sijaona mimba hila hali ambayo nayojiskia kama mtu mjamzito sijapima tena maziwa bado yanauma balaaa sielewi 3
  • @
    @yunnusnassor4938 months ago Mm doctor nimefanya vdond pembn ya chuchu na vnawashs 1
  • @
    @OfficialMariam09-cx4zhlast year Samahani doctor mm ni mjamzito wa miezi 8 lakin napata maumivu makali sana juu ya ziwa lakushoto kiasi kwamba maumiv nayasikilizia kwnenye moyo sasa naomba kujua nini tatizo 2
  • @
    @EsterGeorge-ou1ry9 months ago Dactar ninamaumivu ya matiti nasikia kutapika maumivu ya tumbo la chini linauma kidogo linapoa lakin pia Jana nimeanza kusikia maumivu ya kiuno sijui shida nini 1
  • @
    @grolyyusto2871last year Docta mim niliingia perid trh 30 mwez wa 12 ila mwezi wa kwanz sijaona dumu ila nasikia maumivu chini yatumbo sijapima bad inawez ikawa shida gan nakiuno pia 1
  • @
    @josephcharles84922 years ago Samahan doctor mm ninaujauzito asaivi wa miez miwil na wiki lakini maziwa yangu nilivokuwa na mwezi mmoja na wiki mbili yalikuwa yanauma sana lakina kwa sasa ysmepungua sana kuuma nihali ya kawaida?? 1
  • @
    @slavymwenda64012 years ago Dah ikabid nitafte Mana maziwa yananiuma baraa ni mjamzto wa miezi 3 1
  • @
    @maioscar18099 months ago Mm Nina ujauzito wa miezi 7 lakn maziwa yanawasha hatar shida nn doctor? 1
  • @
    @emilianangava94612 years ago Mi nina mimba ya miezi mitatu mbona maziwa yangu hayatoe majimaji shida ninini na maziwa yarikuwa yanauma sa hivi haya umi? 1
  • @
    @franaelPeter2 weeks ago Doctor samahan Nimeumwa UTI na sjaona period mwez huu wa nne je UTI huweza kusababisha kukosa period
  • @
    @mamag3301last year Happy New Year Doctor Mimi nimepima Nikakuta Na Mimba Ila sina Maumivu yoote ivi Kweli nipo salama au? 1
  • @
    @fridamuss9222 years ago Dokta mm naumwa nina miez 9 ila chuchu zinauma sanaa jamn 1
  • @
    @user-or9kc4xt5m2 months ago Dr kunauwezekano wa siku ya hataree ya 11 kupata mimba, mwenye mzunguko 28 1
  • @
    @angelbaliendez4380last year Samahani naomba kuuliza jisi yakupat mapacha 1
  • @
    @ashaadam12304 months ago Habar dokta mimi titi langu la kulia linawasha nina wiki ya 28 nasugua hadi na brashi hivi kuna tatizo au kuna dawa maana mda mwing nalikuna 1
  • @
    @eneamhume2102last year Dr kwa Nini wakati mwingine tumbo Huwa linapotea linakuwa halionekani kabisa nn tatizo 1
  • @
    @ScolariMadauda-ft1zr7 months ago Chuchu za maziwa zinaniuuma lakini cna dalili yoyote ya ujauzito namaziwa yamejaa kama nina ujauzito 1
  • @
    @jamilajambo1102last year Docta mimi maziwa yanauma alaf maji yanatok kam ya njano na mimba ya miez 6 hiy si kawaida au kuna shida 1
  • @
    @luluhussein5380last year Doctor sorry mim nikijishika kwenye maziw nahis maumivu kwambali nin tatizo 1
  • @
    @lovenessadrian5892 years ago Dr mim napata maumivu ya mgongo kwa chin karbu na kiunon kabsa mbak sas mimba ina miez minne na in mimba yangu ya kwanza 2
  • @
    @hamidatogwa-hu8zylast year Sasa dokta mbn m Toka tendo miezi mitatu lakn mwezi mmoja nimeenda period kama kawaida lakn Toka hapo sijaenda Tena na nilifanya mapenzi wiki ya tatu Kwa mimba kuharibika 2
  • @
    @user-mv6kv9be1d6 months ago Mimi hua sioni period yangu kabisa ni miez ata saba saiv na huwa nikawaida lakin saiv chuchu zinauma je inaweza kua nina ujauzito? 1
  • @
    @vivianotieno34952 months ago Docta mm jaman yananiwasha najikuta najikuna mpk naogopa jmn, nifanyeje? 1
  • @
    @AnnaKombanila19 hours ago Dr hata mimi maziwa yanauma nifanye nini? 1
  • @
    @dullahlitepo1633last year Mimi sio mjamzito ila naumwa matiti na yanawasha na kujaa tatizo litakuwa nini 2
  • @
    @user-zm5bg5hf9i10 months ago Nakama umepoteza ujauzito na maziwa yanamwagika nifanye aje 1
  • @
    @salumsalehe88562 years ago Mm yanakua yananichoma mda hd mda tu so mdawote lkn. Hili lakushoto mda wt linauma ht nikishika je sio shida?? 1
  • @
    @igoberocharlesmogosi22612 years ago Mbona matiti inaniuma bt sina mimba shida n gani? 1
  • @
    @MerySoikan-sr8tl2 months ago Kujaa kwa Matiti Doctor ni dalili ya nn 1
  • @
    @danillarugusha14082 years ago Doctor Mimi nina ujauzito wa miezi 3 ila niki ponda matiti nasikiya kuna mbegu ndani ina mazara gani doctor naomba jibu 1
  • @
    @jamesfety44572 years ago Mimi naumwa na titi la kushoto mpaka kwenye moyo maumivu ni makal mno 1
  • @
    @judyandrew55032 years ago Mama anayenyonyesha matiti kutoa usaha 1
  • @
    @finiasisack33312 years ago Mi Sina hata majimaji na Niko kipindu Cha mwisho shida ni nini 2
  • @
    @magrethsanga56222 years ago Doctor Mimi maziwa yanauma nikipima mimb Sina pia nikiminya yanauma sanaaa Kama wikii mbili sasa 1
  • @
    @user-tk2rx1dk3g9 months ago Doctor chuchu zangu zinauma vibaya hazitoi majimaji lakin zinauma alafu ikifika nyajati za usiku zinavimba sana na nakula mala kwa mala hata 1
  • @
    @shayograce71932 years ago Jamani docta Mimi nawashwa maziwa mpaka nafanya kuyafinya 1
  • @
    @azizarajabu42882 years ago Doctor na maziwa kuuma mpaka kutoka vipele tatizo nn 1
  • @
    @veronicashayo2872 years ago Me matiti yanauma week moja baada ya kufanya ngono...je itakuwa ni mimba au dalili nyngine 1
  • @
    @judykananu40839 months ago Nakama mimba Niya wiki mbili inawesa kuanamaumivu 1
  • @
    @mariumbonifasi72817 months ago Dock msaada mm nili sex siku ya japili nika kabadaya yawiki tena juma pili nikatokwa na dam kidg na chuchu zna uma itakuwa mimba ila nilivo sex nili tumi p2 1
  • @
    @user-lr9lx2nu3k5 months ago Daaaah hapa sichomoi naogopa hata kupima