المدة الزمنية 1:52

UJENZI UWANJA MPYA DODOMA, Waziri Mkuu Majaliwa Awasili Morocco KuwekaMambo sawa

بواسطة BM TV TANZANIA
15 624 مشاهدة
0
66
تم نشره في 2021/07/16

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Tanzania kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) litaendelea kuimarisha mahusiano na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Morocco ili kukuza kiwango cha mpira huo nchini .  Amesema hayo jana (Alhamisi Julai 15, 2021) baada ya kutembelea Ofisi za Shirikisho hilo na eneo la Mchezo wa Mpira wa Miguu la Mohammed wa VI kuona uwekezaji wa miundombinu ya mpira wa miguu uliofanywa katika eneo hilo. Amesema kuwa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Morocco liendelee kutumia fursa ya mafunzo kwa pande zote mbili lengo likiwa ni kuwa na timu za taifa zilizo bora na zenye ushindani kama ilivyo kwa timu ya taifa ya Morocco. Aliongeza kuwa shirikisho hilo limekuwa likiisadia sana Tanzania katika kujifunza mbinu mbalimbali za kiutawala pamoja na mbinu za kimichezo kupitia timu za taifa za Tanzania.

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 1