المدة الزمنية 18:37

Exclusive Interview: Huyu Ndiye Anayempa Jeuri Harmorapa

بواسطة Global TV Online
59 869 مشاهدة
0
397
تم نشره في 2017/02/28

Wengi wanashangazwa na mafanikio ya ghafla ya msanii wa muziki wa kizazi kipya, aliyejipatia umaarufu mkubwa kutokana na kufananishwa na memba wa WCP, Harmonize, Harmorapa, lakini je, unajua nani yupo nyuma yake? Mara kwa mara Harmonize amekuwa akionekana akipiga picha na maburungutu ya fedha na hivi karibuni, alikabidhiwa gari na bosi wake. Unamjua bosi mwenyewe ni nani? Global TV Online imefanikiwa kukutana na Irene Sabuka, mfanyabiashara wa spea za magari, mwenye ofisi zake Kariakoo ndiye anayempa jeuri ya fedha Harmorapa. Ndani ya video hii, anaeleza ni jinsi gani alikutana na Harmorapa na namna anavyomsimamia kimuziki. Mwanamama Irene anasema kwamba alikutana na Harmorapa, Mwenge jijini Dar es Salaam, jamaa akiwa anauza pochi ambapo Irene akiwa anamuungisha pochi moja, alisikia vijana wenzake wakimuita kwa jina la Harmonize. Akaamua kumuagiza pochi nyingine na huo ukawa mwanzo wa wawili hao kufahamiana, ambapo baadaye Harmorapa alifunguka kwamba anaweza kuimba, akamsikilizisha kazi zake na baada ya hapo, wakakubaliana kwamba Irene ndiyo awe msimamizi wake wa kazi za sanaa. By KASMIR MSELECHE

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 90