المدة الزمنية 15:25

UFAFANUZI- Mgodi wa Nyamongo wapigwa faini ya Bilioni 5.6

بواسطة BMG Online TV
5 177 مشاهدة
0
17
تم نشره في 2019/05/17

******************************************************************************* Serikali kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), imeupiga faini ya shilini bilioni 5.6 mgodi wa dhahabu wa Acacia North Mara uliopo Nyamongo wilayani Tarime, kwa kushindwa kudhibiti bwawa la maji yenye sumu na hivyo kuhatarisha afya za wakazi wanaozunguka mgodi huo. Maamuzi hayo yalitolewa jana baada ya Waziri wa Madini, Doto Biteko pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba kufanya ziara mgodini hapo, wakiambatana na Watendaji mbalimbali. Faini hiyo ilitangazwa na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Samuel Gwamaka baada ya ripoti ya Kamati Huru iliyoundwa kwa ushirikiano wa Wizara mbalimbali ikiwemo Wizara ya Madini, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Maji, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) pamoja na Wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam kubaini mgodi huo umekuwa ukitiririsha maji yenye sumu kwa zaidi ya miaka 10 huku ukitoa taarifa zenye udanganyifu kuhusiana na maji hayo. Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 3