المدة الزمنية 4:51

Mafua ya Kuku (Infectious Coryza) - Kusafisha Jicho na Tiba

بواسطة Changamkia Fursa
19 687 مشاهدة
0
127
تم نشره في 2021/11/14

Mafua ya Kuku (Infectious Coryza) - Jinsi ya kusafisha jicho, Dalili na Tiba Ni ugonjwa unaosababishwa na bacteria ambao hushambulia zaidi kuku na ndege wa porini. Ugonjwa, hushambulia kuku wa umri wowote. Chanzo cha maambukizi ni maji na chakula kilichochafuliwa na kinyesi cha kuku wagonjwa. Kuku au ndege wagonjwa huambukiza wenzao kupitia mfumo wa hewa wanapopiga chafya. Dalili 1. Ugonjwa huu hushambulia zaidi mfumo wa hewa na hivyo kusababisha dalili zifuatazo: 2. Makamasi mazito yenye usaha hutoka puani 3. Kuku anashindwa kupumua, hukohoa na kupiga chafya 4. Harufu mbaya kutoka kinywani 5. kuvimba jicho na kuweka uchafu kama maziwa yaliyoganda 6. Jicho kutoa machozi au vipovu kwenye Kona za jicho 7. Vifo vya kuku vinaweza kufikia asilimia 20 Dawa ambazo naweza kukushauri uwapatie kuku wako ni hizi zifatazo.. 1.Mafua ya awali ambayo hayaja ambatana na vifo wape FLUBAN 2. Mafua ambaya yameambatana na vifo wape ENROVET au TYLODOX Kujiunga Pdf (eBook) ya Muongozo wa UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI bonyeza link na fata Maelekezo bit.ly/3Dhv4mc

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 23