المدة الزمنية 1:40

MZOZO WA PALESTINA NA ISRAEL: GHOROFA LENYE OFISI ZA ALJAZEERA,AP LALIPULIWA, WALIONYWA “KUNA VIFO

بواسطة Millard Ayo
38 696 مشاهدة
0
268
تم نشره في 2021/05/16

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema ameshangazwa na mashambulizi yanayoendelea Palestina dhidi ya Raia na kusikitishwa na kushambuliwa kwa Jengo la ghorofa mjini Gaza, lenye Ofisi za Vyombo vya Habari vya Associated Press (AP) na Al Jazeera ambalo limeanguka baada ya kupigwa na shambulio la roketi iliyofyatuliwa na Ndege ya Israeli. Mlipuko huo haujaleta madhara makubwa kwakuwa Wafanyakazi wengi wa Vyombo hivyo vya Habari walikua tayari wameondoka kwenye jengo hilo kabla ya mlipuko, baada ya Mmiliki wake kupata onyo kutoka kwa Israeli mapema juu ya mashambulizi. Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric, amesema Guterres amefadhaishwa na shambulizi la anga la Israel lililofanywa jana katika jengo hilo na pia amesikitishwa na vifo vya Watu 10 wa Familia moja pamoja na Watoto vilivyotokea katika shambulizi jingine la usiku wa Ijumaa. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linakutana leo kuujadili mzozo kati ya Israel na Palestina, huku Viongozi wa Mataifa mbalimbali wakielezea wasiwasi wao baada ya mashambulizi hayo ya Israel ambayo yamewaua pia Watoto wanane

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 222