المدة الزمنية 6:11

Hii Ndiyo Siri Kubwa Ya Waandishi Wenye Mafanikio Makubwa

بواسطة Dr. Makirita Amani
2 596 مشاهدة
0
43
تم نشره في 2017/08/10

Rafiki, Wahenga walisema ukiona vyaelea ujue vimeundwa. Dunia inapenda kuona matokeo, lakini haipendi kuona ule mchakato wa matokeo hayo, namna gani yamefikiwa. Huwa tunaona habari za watu waliotoka chini kabisa na kufanikiwa sana, lakini hatupati ile picha halisi ya njia walizopita mpaka wakafanikiwa. Utasikia maneno kwamba alikazana sana na hakukata tamaa, mwishowe amefanikiwa. Lakini huenda huko katikati mtu alikata tamaa kwenye mambo mengi. Huenda mpango aliokuwa nao mwanzo siyo huo ambao amefanikiwa nao. Huenda kuna mahali alivunja sheria, alikiuka taratibu na alifanya mambo ambayo kikawaida hayawezi kukubalika, lakini yakamwezesha kuvuka hatua moja kwenda nyingine. Ninachotaka kukuambia ni kwamba, kuna safari ndefu na ngumu ya kufika popote ambapo mtu anataka kufika. Kwenye uandishi napo mambo yako hivyo hivyo. Wapo waandishi wenye mafanikio makubwa, walioandika vitabu vingi ambavyo vimegusa maisha ya wengi. Lakini wengi wamekuwa wanaviona vitabu pekee, hawaoni maisha nyuma ya vitabu hivyo. Wengi wamekuwa wanafurahia mafanikio ya waandishi wenye mafanikio, na wao kukimbilia kuandika, bila ya kujua kazi kubwa iliyopo nyuma ya uandishi wenye mafanikio. Mmoja wa waandishi ninaowakubali sana, alikuwa anahojiwa, akaulizwa mchakato wake wa uandishi wa vitabu ukoje. Akajibu bila ya kusita kwamba kabla hajaandika kitabu kimoja, basi anasoma vitabu 250, ndiyo vitabu mia mbili na hamsini. Unaweza kuona namna gani hiyo kazi siyo ndogo wala rahisi, hapo ni kusoma na hata hajaanza kuandika. Kwenye kipindi cha leo nimekuandalia somo kuhusu siri kubwa ya waandishi wenye mafanikio makubwa. Angalia kipindi hichi kujifunza kitu muhimu unachopaswa kukipa kipaumbele kama unataka kufanikiwa kwenye uandishi. Na hata kama wewe siyo mwandishi, angalia kipindi hichi, kitakupa funzo kubwa la namna unavyopaswa kujitoa kwa ajili ya mafanikio. Kocha Makirita Amani.

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 5