المدة الزمنية 27:4

INATISHA Baada ya Kutoka Jela, Rama Mla Watu Afunguka Jinsi Alivyokamatwa Akila Kichwa cha Mtoto

بواسطة Global TV Online
1 240 091 مشاهدة
0
3.8 K
تم نشره في 2017/06/17

Rama Mla Vichwa Vya watu ni stori iliyotawala vyombo vyabari nchini Tanzania mwaka 2008 baada ya kijana huyo kukamatwa akiwa na kichwa cha binadamu cha mtoto Salome, ambacho alikuwa akikinyonya damu. Kwa kumbukumbu, mwaka 2008, akiwa na umri wa miaka 11 tu, Rama alishikiliwa na vyombo vya dola nch­ini Tanzania kwa tuhuma za mauaji ya mtoto, Salome Yohana (3), mkazi wa Tabata jijini Dar, baada ya kuku­twa na kichwa cha mtoto huyo kiki­vuja damu huku akikitafuna katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar, yapata miaka tisa iliyopita. Mwaka 2013, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ilimuachia huru Rama kufuatia ripoti ya daktari iliyoonesha kuwa wakati anatenda kosa hilo alikuwa ana matatizo ya akili. Tofauti na wafungwa wengine am­bao wakiachiwa huru hurudi mtaani, Rama alipelekwa katika Hospitali ya Watu Wenye Matatizo ya Akili ya Mirembe mkoani Dodoma kwa kuwa ilibainika ana matatizo ya akili. Mapema wiki hii GLOBAL TV ONLINE ilipata nafasi ya kuongea naye ana kwa ana na kufunguka mengi. www.globaltvtz,com www.globalpublishers.co.tz www.facebook.com/globalpublishers www.instagram.com/globalpublishers

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 769