المدة الزمنية 57:15

Rais Magufuli alipozindua Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu DSM

بواسطة Azam TV
5 828 مشاهدة
0
26
تم نشره في 2018/04/11

Ziko hapa hotuba kamili walizozitoa Rais Magufuli na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete. Ni hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete, iliyo chini ya Rais wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Ikulu Dar es Salaam leo tarehe 11 Aprili, 2018. Mgeni rasmi katika shughuli hii ni Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ambaye katika hotuba yake amempongeza rais mstaafu Jakaya Kikwete kwa kuzindua taasisi hiyo na kumuahidi ushirikiano na kuwaomba wahisani kushirikiana naye. Katika hotuba yake Rais Magufuli amewataka Watanzania kuwaenzi viongozi wastaafu na kusema kuwa huwa anafarijika anapokuwa amekutana na viongozi hao wastaafu. "Tanzania ni nchi ya kuigiwa mfano, ninafarijika sana ninapokuwa nimekutana na wazee hawa, huku mzee Mwinyi, Mkapa na Kikwete na huku makamu wa marais na mawaziri wakuu, wapo wanaopenda kuchonganisha lakini napenda kusema, ninyi wastaafu mfurahie maisha..." "Huwa ninasoma na kuyaangalie yanayosemwa lakini nayaacha tu.." Aidha amekemea na kuendelea kusisitiza kuwa hatokaa ashirikiane na taasisi zenye malengo ya kuchafua serikali na kuvuruga amani ya nchi.

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 2